Ebay ni sehemu ambayo wauzaji na wanunuaji wanakutana
Muuzaji anajiunga kwa kufungua Account ebay na kisha anatangaza kitu anachokiuza akiwa popote pale Duniani
Mnunuzi anajiunga kwa kufungua Account ebay popote alipo Duniani kisha anachagua bidhaa anayoitaka iliyotangazwa na Muuzaji(Seller) ana inunua online.
MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUTUMIA EBAY
1. Tafuta Debit card au Credit card
Debit card ni kadi inayokuwezesha kununua vitu kwenye mtandao kwa
kutumia pesa iliyo kwenye akaunti yako ya benki. Na Credit card
inakuwezesha kununua kwa kukopa kwenye benki unayotumia halafu
wanakukata kidogokidgo kwenye mshahara wako au namna yoyote ambayo
mtakubaliana na benki. Kadi hizi ni kama Tembo card visa na Tembo card
master card za CRDB Bank;
benki zingine kama NBC, Stanbic Bank na BARCLAYS Bank pia zinatoa Kadi
Za namna hiyo. Baada ya kupata kadi yako unatakiwa uende kwenye benki
yako wakairuhusu kuweza kufanya manunuzi kwenye mtandao.
2. Jiunge na tovuti ya Paypal.
Paypal ni tovuti inayoongoza duniani kwa kusimia malipo ya kwenye
mtandao. Kazi yake kubwa ni kutunza taarifa zako muhimu za benki ili
wamachinga wa kwenye mtandao wasizizoee hovyo. Hivyo basi ukitumia
paypal, unasajili na kuweka namba yako ya visa au master card.
Baada ya hapo unaweza kuweka pesa kwenye account ya paypal au ukaziacha
kwenye akaunti yako ya benki. Unapofanya manunuzi Yule muuzaji anapewa
pesa na Paypal sio wewe moja kwa moja ili kulinda taarifa zako za benki.
3. Nunua kwenye tovuti iliyo na mfumo wa kutuma taarifa zako kwa usalama.
Kwa ajili ya usalama kuna teknologia inaitwa SSL(Secure Socket Layer).
SSL inafanya kazi ya kusafirisha taarifa zako katika hali ya mkanganyiko
ili mtu yoyote mhalifu asiweze kuzielewa, zikifika zianaundwa tena ili
muuzaji aweze kuzielewa.
Teknologia hii inatumika pia kutuma email, blackberry wakiwa ni vinara
wa kutunia teknologia hii. Ili kujua kama tovuti inatumia hii teknologia
utaona alama ya kufuli kwenye anuani ya tovuti husika ikishafunguka.
Angalia kwenye sehemu ya kuandikia anuani, kushoto au kulia.
4. Nunua kwa muuzaji anayekubaliwa na weteja wengi.
Utajuaje kama muuzaji anakubalika sokoni na anauzoefu wa kuuza vitu
kwenye mtandao? Rahisi! Kwa mfanounataka kununua saa Ebay au kitabu cha
electrniki (PDF) kwenye Amazon, chini ya hiyo bidhaa iliyoichagua utaona
maoni ya watu walionunua kabla yako.
Ni vizuri ukatumia muda wa kutosha kusoma maoni ya waru wengi kabla
hujaendelea za zoezi la manunuzi. Njia nyingine ya kupata maoni ya watu
ni kutumia tovuti kama Yelp, Google+, Yahoo directory au Yellow pages
iwapo muuazaji atakuwa amejiunga nazo.
5. Chagua namna ya kutumiwa mzigo wako.
Unatakiwa kuchagua namna kutumiwa mzigo wako ambayo itakuwa rahisi kwako
kuupata. Gharama za kutuma mzigo zitaoneshwa pale kwenye mtandao na
muda wa kufika kwa kila gharama. Kwa Tanzania unaweza kutumia DHL, UPS
au shirika lolote unaloliamini.
6. Hakikisha muuzaji anahudumia eneo ulilopo.
Baadi ya wauzaji huchagua nchi au miji wanayoweza kutuma mizigo na
wengine huuza dunia nzima. Taarifa hizi huwekwa chini ya bidhaa
unayotaka kununua , hii itakusaidia kuokoa muda kuondoa usumbufu usio wa
lazima.
Pia waweza tumia njia hizo kwa mitandao mengine tofauti na ebay ila zingatia:
Unaponunua kitu kwenye mtandao kwanza kabisa hakikisha hiyo tovuti
inafahamika, kama haifahamiki hakikisha kuwa imethibishwa na na
mashirika yakuhalalisha biashara za kwenye mtandao kama BBB (Better
Business Bureau), utaona nembo ya haya mashirika chini kwenye tovuti ya
muuzaji.
kwa mungozo zaiidi na maswali bonyeza hapa
Wednesday, 30 September 2015
Home »
» JIFUNZE NAMNA YA KUFANYA MANUNUZI EBAY
0 comments:
Post a Comment