Tuesday 12 January 2016

JINSI YA KUANGALIA SIMU KAMA NI FEKI

Makala hii itakuonesha jinsi ya kuangalia kama simu yako ni feki ama la. Zifuatazo ni hatua unazoweza kuzitumia kuangalia kama simu yako ni feki, hakuna mahitaji makubwa kufanya hili ila tu unahitaji simu yako unayoitumia na unayotaka kuiangalia. Jinsi ya angalia IMEI namba Andika *#06# kisha bonyeza kitufe cha kupiga Baada ya hapo simu yako itakuletea IMEI namba ambapo kama simu yako au kifaa chako kina laini mbili basi kutakuwa na IMEI namba mbili Namba hii pia unaweza kuipata katika boksi la simu ama nyuma ya ya simu hiyo baada ya kutoa betri, utaijua kwa kuwa huwa ni tarakimu 15. Nakili namba hizo pembeni. Jinsi ya kuangalia kifaa kama ni feki ama halali Iandike ile namba uliyo nakili katika hatua iliyopita katika sehemu ya kuandikia ujumbe (SMS) Utume ujumbe huo kwenda namba 15090 Baada ya kutuma meseji hiyo utaangaliziwa je hiyo IMEI namba ni ya simu ya aina gani na nani mtengenezaji wa simu hiyo. Subiri majibu (haitachukua muda mrefu) Ujumbe huo ukija unakuwa na maelezo ya kampuni iliyotengeneza simu hiyo pamoja na jina la simu hiyo. jinsi ya kuaangalia simu kama feki Mfano wa ujumbe unarudishwa baada ya kutuma IMEI namba Jinsi ya kujua kama simu yako ni feki Kama jina la mtengenezaji wa simu yako pamoja na aina ya simu yako (Uliyo jibiwa baada ya kutuma IMEI namba) haviendani na majina ya simu yako (ambayo yameandikwa katika simu yako) basi ujue simu yako inamashaka na ni vyema kumuuliza muuzaji wako juu ya hilo. Kama majina yaliyorudi hayaendani na majina yaliyoandikwa katika simu yako basi upo katika kundi lenye uwezekano wa kuwa na matatizo, TUNAKUSHAURI ufuate utaratibu na kuibadilisha ama kuacha kuitumia simu hiyo kabla ya mwezi Juni. Kwanini TCRA wanataka tubadilishe simu Simu isiyo na IMEI ni sawa na gari lisilo na namba za usajili {plate number} Vyombo vya usalama vinaweza kukamata wahalifu wa kutumia mitandao ya simu kwa msaada wa IMEI namba hivyo mtu akiwa anatumia simu ambayo haina au ina IMEI namba ambayo sio sahihi anazuia utendaji kazi wa taasisi za usalama hivyo wao kama mamlaka wanatakiwa kuhakikisha kila mtu anatumia simu yenye IMEI namba sahihi.
Share:

Saturday 9 January 2016

Ifahamu simu janja yenye uwezo wa kukaa na chaji zaidi ya siku kumi

Simu janja yenye uwezo wa kukaa na chaji kwa zaidi ya siku 10? Haraka haraka jambo hili linaonekana bado ni ndoto ila tayari kuna kampuni ambayo imedai imefanikisha jambo hili na simu zake zitaanza kupatikana mapema mwezi wa kwanza, 2016. Simu janja hiyo inakuja na betri lenye kiwango kikubwa cha uhifadhi chaji wa mAh 10,000 italetwa na kampuni iitwayo Oukitel. Wenyewe wanasema kwa matumizi ya ‘kawaida’ wanategemea simu hiyo iweze kukaa na chaji kwa zaidi ya siku 10, wanasema kutegemea na utumiaji inaweza fikisha hadi siku 15. Oukitel K10000Oukitel K10000 Kampuni hiyo tayari miezi kadhaa nyuma ilishawahi kutoa simu janja yenye kiwango kikubwa cha uhifadhi chaji wa mAh 6000. Simu hii ya kiwango cha chaji cha mAh 10,000 itachukua jina la Oukitel K10000 na inakuja ikitumia toleo la Android 5,1 Lollipop. Kupitia simu hiyo utaweza pia kuitumia kama vile ‘powerbank’ ili kuweza kuchaji simu yako nyingine ya ziada. :-) Sifa zinginezo za Oukitel K10000 Kioo (display) ya Inchi 5.5 HD (720X1280) Prosesa – 1GHz quad-core MediaTek MT6735 RAM GB 2 Diski Uhifadhi (Storage) – GB 16 na uwezo wa kutumia kadi ya microSD Kamera ya mbele ya MegaPixel 8 na ya selfi MegaPixel 2 Kamera ya mbele inakuja na teknolojia za HDR, kutambua sura (face detection), uwezo wa kupiga picha za panorama n.k Kimawasiliano inakuja na teknolojia za GPRS/EDGE na 3G, pia Bluetooth na WiFi. Kwa sasa simu hiyo ishaanza kuuzwa kupitia mtandao wa GearBest kwa takribani dola 240 za Marekani, wanaolipia kwa sasa wataanza kuipata simu hiyo mwezi wa kwanza ambapo ndio pia itaanza kupatikana katika nchi zingine.
Share:

nature beauty

Powered by Blogger.

recent posts

Total Pageviews

Search This Blog

technology

Number of Posts

featured video

Random Post Number

Slider Display

Random

The Slider

social counter

twocolumns

about us

About

Formulir Kontak

Name

Email *

Message *

Social Icons

Featured Posts

FOLLOW @ INSTAGRAM

Must read